• HABARI MPYA

  Monday, July 09, 2018

  SALUM MAYANGA AREJEA MTIBWA SUGAR, SAFARI HII NI KAMA MKURUGENZI WA UFUNDI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kumaliza mkataba wa kuitumikia timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Kocha Salum Mayanga amerejea kwenye klabuu yake ya zamani Mtibwa Sugar kama Mkurugenzi wa Ufundi.
  Salum Mayanga kabla ya kuitumikia Taifa Stars, alikuwa mchezaji na baadaye kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar na sasa anarejea kama Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya kikosi hicho. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online, Katbu Msaidizi wa klabu hiyo, Abubakar Swaburi amesema kwamba dhumuni la kumrejesha Kocha Mayanga ndani ya Mtibwa Sugar ni kuimarisha sekta ya benchi la ufundi.

  Katbu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swaburi (kulia) akimtambulisha Salum Mayanga baada ya kurejea rasmi leo 

  "Lengo la kumrejesha Kocha Salum Mayanga ni kutaka kuimarisha sekta ya benchi la ufundi kwa sababu benchi la ufundi linamambo mengi makocha pekee hawawezi kujitosheleza kila kitu hivyo tumemuajiri kama mkurugenzi wa ufundi wa Mtibwa na cheo hiki hakikuwepo awali lakini tumemteua yeye ili afanye majukumu ya mkurugenzi wa ufundi" amesema Swabur.
  Kiongozi huyo ameongeza kwamba Zuberi Katwila ataendelea kuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Patrick Mwangata ambaye pia ni Kocha wa Makipa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALUM MAYANGA AREJEA MTIBWA SUGAR, SAFARI HII NI KAMA MKURUGENZI WA UFUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top