• HABARI MPYA

  Tuesday, July 10, 2018

  REAL MADRID YAKUBALI KUMUUZA RONALDO JUVENTUS PAUNI MILIONI 88

  MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo anaweza kuondoka Santiago Bernabeu kujiunga na Juventus ya Italia kwa dau la Pauni Milioni 88 baada ya klabu yake, Real Madrid kukubali kumuuza.
  Ronaldo amekutana na Rais wa Juventus, Andrea Agnelli leo mchana hotelini nchini Ugiriki kabla ya kukubali mshahara wa Pauni 500,000 kwa wiki kuhamishia huduma zake Turin.
  Na ni kikao hicho inaaminika kimekamilisha mpango huo wa Ronaldo aliye mapumzikoni na familia yake, mpenzi wake na wanawe kuhamia Italia. 
  Na tayari Real Madrid imethibitisha uhamisho huo mchana wa leo katika taarifa iliyoitoa ikisema wanatarajia Ronaldo ataihama klabu hiyo.

  Cristiano Ronaldo anaondoka Real Madrid ya Hispania kuhamia Juventus ya Italia 


  Taarifa imesema: "Leo, Real Madrid inataka inataka kuelezea kuhusu mchezaji ambaye amethibitisha kuwa bora duniani na ambaye ameng'ara mno kwenye historia ya klabu yetu na dunia ya soka,." 
  Ronaldo ameshinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa katika miaka yake tisa ya kuwa na Real Madrid. 
  Pamoja na mafanikio yake ikiwemo kushinda mataji katika miaka hiyo tisa, Ronaldo pia amekuwa mfano kwa kipaji chake, uwajibikaji, kujitolea, kujituma na kadhalika.
  Kwa upande wake, Ronaldo ameishukuru Real Madrid kwa kumfanya awe na wakati mzuri katika klabu hiyo.
  "Naamini kwamba wakati umefika nifungue ukurasa wangu mpya katika maisha yangu na ndiyo maana nimeiomba klabu ikubali kunihamisha. Nimefikiri hivyo na nimemuuliza kila mmoja, na hususan mashabiki wangu, tafadhali wanielewe,"amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAKUBALI KUMUUZA RONALDO JUVENTUS PAUNI MILIONI 88 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top