• HABARI MPYA

  Monday, July 09, 2018

  KIUNGO WA URUGUAY ATHIBITISHA KWENDA KUFANYA VIPIMO ARSENAL

  KIUNGO  wa ulinzi wa Uruguay, Lucas Torreira amethibitisha kuwa njiani kwenda kufanya vipimo vya afya tayari kujiunga na Arsenal.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameng'ara kwenye Fainali za Kombe la Dunia akiwa na Uruguay iliyofika Robo Fainali na kutolewa na Ufaransa Ijumaa.
  Na klabu yake ya sasa, Sampdoria imekubali ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25 kutoka Arsenal katika mazungumzo yaliyofanyika wakati akiwa Urusi kwenye Kombe la Dunia.

  Lucas Torreira amethibitisha kuwa njiani kwenda kufanya vipimo vya afya tayari kujiunga na Arsenal 

  Torreira anaelekea kuwa mchezaji wa nne mpya kusajiliwa Arsenal chini ya kocha mpya, Unai Emery aliyejiunga na timu Juni kuchukua nafasi ya kocha wa muda mrefu, Mfaransa, Arsene Wenger.
  Kocha huyo wa zamani wa PSG na Sevilla tayari amewanasa kipa Bernd Leno, beki Stephan Lichtsteiner na Soktratis Papasthathopoulous.
  Kwa misimu mitatu iliyopita Torreira amekuwa akichezea kikosi cha kwanza cha Sampdoria baada ya kuibukia akademi ya timu, Pescara.
  Mechi ya kwanza ya Emery Arsenal itakuwa ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Atletico Madrid, Julai 26. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO WA URUGUAY ATHIBITISHA KWENDA KUFANYA VIPIMO ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top