• HABARI MPYA

    Tuesday, July 17, 2018

    KILIMANJARO QUEENS WAANZA KUJIFUA KIGALI TAYARI KUTETEA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE

    Na Mwandishi Wetu, KIGALI
    TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens leo imefanya mazoezi yake ya kwanza mjini Kigali, Rwanda tayari kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kwa wanawake.
    Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo imesema kwamba mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha Mkuu Bakari Shime yamefanyika kwenye Uwanja wa Mumena uliopo Nyamirambo.
    Wachezaji wote wameshiriki kikamilifu katika mazoezi hayo yaliyoanza saa 2 na nusu asubuhi kwa saa za hapa Rwanda sawa na saa 3 na nusu kwa nyumbani Tanzania.

    Kilimanjaro Queens ipo nchini Rwanda kwa ajili mashindano ya CECAFA kwa Wanawake 
    Kilimanjaro Queens inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya wenyeji Rwanda Alhamis Julai 19.
    Kikosi hicho kina jumla ya wachezaji 20 na viongozi 5 wa benchi la Ufundi ambao ni Stumai Abdallah, Asha Hamza, Asha Rashid, Enekia Kasongo, Gerwa Yona, Fatuma Issa, Amina Ally na Mwanahamis Omary.
    Fatuma Mustafa, Fatuma Omary, Ester Mayala, Eveline Sekikubo, Happy Hezron, Fatuma Abushiri, Fatuma Hassan, Maimuna Mainuna Khamis, Donisia Daniel, Wema Richard, Najiath Idrissa na Fatma Khatib.
    Viongozi wa benchi la Ufundi ni kocha Mkuu Bakari Shime, Kocha msaidizi Edina Lema, Kocha wa makipa Eliuter Mollel, Daktari Blandina Mnambya na meneja wa vifaa Ester Chabruma.
    Kiongozi wa msafara ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Issa Bukuku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS WAANZA KUJIFUA KIGALI TAYARI KUTETEA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top