• HABARI MPYA

    Thursday, July 12, 2018

    KILA KLABU LIGI KUU YARUHUSIWA KUSAJILI HADI WACHEZAJI 10 WA KIGENI KUANIZA MSIMU UJAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeongeza idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutoka saba hadi 10 kuanzia ujao wa 2018/2019.
    Hayo yamesemwa leo mchana na Rais wa TFF, Wallace Karia alipokuwa akizungumzia masuala mablimbali ya soka nchini katika mkutano wake na Waandishi wa Habari.
    Lakini Karia akasema suala la kuongeza wachezaji 10 wa kigeni litatolewa ufafanuzi baadaye lakini leo alikuwa anathibitisha tu.
    Pamoja na hayo, Karia leo ametangaza kumvua Uenyekiti wa Bodi ya Ligi, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 
    Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

    Mshambuliaji Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi akimiliki mpira mbele ya beki Mghana wa Azam FC, Yakubu Mohamed msimu ulilopita

    Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.
    "Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia 
    Katika hatua nyingine, Karia amesema Kamati ya Utendaji imempitisha rasmi Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kukaimu kwa muda mrefu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILA KLABU LIGI KUU YARUHUSIWA KUSAJILI HADI WACHEZAJI 10 WA KIGENI KUANIZA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top