• HABARI MPYA

    Thursday, July 12, 2018

    KARIA AMVUA SANGA UENYEKITI WA BODI YA LIGI, ASEMA HANA SIFA...KIDAU APEWA 'ULAJI' RASMI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Sheria na Katiba ya kumsimamisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 
    Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

    Rais wa TFF, Wallace Karia (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam

    Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.
    "Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia 
    Katika hatua nyingine, Karia amesema Kamati ya Utendaji imempitisha rasmi Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kukaimu kwa muda mrefu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KARIA AMVUA SANGA UENYEKITI WA BODI YA LIGI, ASEMA HANA SIFA...KIDAU APEWA 'ULAJI' RASMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top