• HABARI MPYA

  Wednesday, July 11, 2018

  KAGERE AIPELEKA SIMBA SC FAINALI KOMBE LA KAGAME…ITAKUTANA NA AZAM IJUMAA TAIFA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inakwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame na itakutana na Azam FC katika fainali Ijumaa hapa hapa Uwanja wa Taifa.
  Kagere aliyesajiliwa mwezi uliopita kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi baada ya kupokea pasi mshambuliaji Mghana, Nicholas Gyan anayetumika kama beki kwa sasa.
  Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akimuacha chini beki wa JKU leo Uwanja wa Taifa
  Meddie Kagere akinyoosha mkono juu baada ya kuifungia Simba SC bao pekee leo

  Pamoja na ushindi huo, Simba SC ilipata wakati mgumu kwa vijana wa Jesho la Kujenga Uchumi (JKU) waliokuwa wakiongozwa vizuri na kiungo hodari, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
  Ikumbukwe katika Nusu Fainali ya kwanza, Azam FC ilishinda 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa pia, mabao ya mshambuliaji mpya, Ditram Nchimbi dakika ya 92 na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa dakika ya 100.
  Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Paul Bukaba, James Kotei, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk64, Mwinyi Kazimoto, Meddie Kagere, Mohammed Rashid/Moses KItandu dk89 na Marcel Kaheza/Rashid Juma dk78. 
  JKU:  Mohammed Abrahman, Issa Haidar Dau, Edward Peter, Mwinjuma Mwinyi, Salum Said, Faisal Salum, Ali Vuai/Amour Suleiman dk58, Nassor Mattar, Abrahman Mussa, Suwed Juma na Khamis Abdallah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERE AIPELEKA SIMBA SC FAINALI KOMBE LA KAGAME…ITAKUTANA NA AZAM IJUMAA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top