• HABARI MPYA

  Saturday, July 07, 2018

  JKT QUEENS WACHUKUA UBINGWA LIGI YA WANAWAKE WAKISHINDA MECHI ZOTE, LEO WAMEMALIZIA KWA KUIPIGA 6-2 MLANDIZI QUEENS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya JKT Queens imefanikiwa kutewaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara kwa kishindo, baada ya kumaliza na pointi 42 kutokana na kushinda mechi zake zote 14.
  Hiyo ni kufuatia ushindi wa mabao 6-2 jioni ya leo dhidi ya wenyeji, Mlandizi Queens Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani katika mchezo wa kufunga pazia la ligi hiyo hatua ya mwisho ya Nane Bora.
  Mabao ya JKT Queens leo yamefungwa na Donisia Minja, Fatuma Mustapha, Wema Maile aliyejifunga, Stumai Athuman, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Fatuma Mustapha, wakati ya Mlandizi Queens yamefungwa na Jamila Hassan na Mwanahamis Omary ‘Gaucho’.
  Mechi nyingine za leo, Kigoma Sisters imeshinda 4-0 dhidi ya Evergreen na Panama imeilaza 3-2 Alliance na Baobab imeifunga 4-1 Simba Queens.
  Kigoma Sisters imemaliza katika nafasi ya pili kwa pointi zake 30, ikifuatiwa na Alliance Girls pointi 24 na waliokuwa mabingwa watetezi, Mlandizi Queens walioambulia pointi 22.


  JKT Queens iwakifurahia baada ya kukabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara leo Mlandizi


  MSIMAMO KAMILI NANE BORA LIGI YA WANAWAKE:

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT QUEENS WACHUKUA UBINGWA LIGI YA WANAWAKE WAKISHINDA MECHI ZOTE, LEO WAMEMALIZIA KWA KUIPIGA 6-2 MLANDIZI QUEENS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top