• HABARI MPYA

  Sunday, July 08, 2018

  HASSAN BANYAI KOCHA MPYA PAMBA SC…APEWA JUKUMU LA KUIREJESHA TP LINDANDA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  KATIKA kuhakikisha inafanya vizuri kwenye Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara na kurejea Ligi Kuu, klabu ya Pamba FC ya mjini Mwanza imemchukua Hassan Banyai kuwa kocha wake Mkuu kwa msimu wa 2018/2019.
  Banyai, mchezaji wa zamani wa timu ya mkoa wa Dar es Salaam ‘Mzizima United’, anajiunga na Pamba FC, mabingwa wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  Afisa Habari wa klabu ya Pamba FC, Johnson James amesema kwamba uongozi wa klabu umevutiwa na rekodi ya kocha huyo na una matumaini makubwa ya kurejea Ligi Kuu klabu yao timu ikinolewa na Banyao.

  Hassan Banyai ameingia mkataba wa mwaka na Pamba FC kwa msimu wa 2018/2019

  Hatua ya klabu hiyo kumchukua kocha huyo inapongezwa na katibu mkuu wa chama cha Soka Mwanza (MZFA), Leonard Malongo ambaye pamoja na mambo mengine ameeleza mkakati wa MZFA katika kuzisaidia klabu za Mwanza kufanya vyema katika mashindan mbalimbali.
  Kwa taklibani miaka 18 Klabu ya Pamba ya jijini hapa imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inarejea Ligi Kuu bila mafanikio, hatua ambayo hata hivyo haiwakatishi tamaa wadau wa klabu hiyo katika kuiunga mkono klabu hiyo.
  Pamba ilikuwa timu tishio katika soka ya Tanzania tangu miaka ya 1970 kabla ya kuja kupewa jina la utani, TP Lindanda miaka ya 1980 mwishoni na sasa inataka kurejea Ligi Kuu kupitia kwa Banyai, kocha wa zamani wa Njombe Mji FC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HASSAN BANYAI KOCHA MPYA PAMBA SC…APEWA JUKUMU LA KUIREJESHA TP LINDANDA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top