• HABARI MPYA

  Sunday, July 08, 2018

  CROATIA YAWANG'OA WENYEJI URUSI KWA MATUTA, KUKUTANA NA ENGLAND NUSU FAINALI

  Wachezaji wa Croatia wakikimbia kushangilia baada ya ushindi wa penalti wa 4-3 kufuatia sare ya 2-2 na wenyeji, Urusi usiku huu katika mchezo wa mwisho wa Robo Fainali ya Kombe la Dunia Uwanja wa Olimpiki mjini Fisht, Sochi. Mabao ya Urusi yalifungwa na Denis Cheryshev dakika ya 31 na Mario Fernandes dakika ya 115, wakati ya Croatia yalifungwa na Andrej Kramaric dakika ya 39 na Domagoj Vida dakika ya 100.
  Penalti za Urusi zilifungwa na Alan Dzagoev, Sergei Ignashevich na Daler Kuzyaev, wakati Fyodor Smolov  na Fernandes walikosa huku za Croatia zikifungwa na Marcelo Brozovic, Luca Modric, Vida na Ivan Rakitic. Croatia sasa itakutana na England katika Nusu Fainali Jumatano, wakati Ufaransa itamenyana na Ubelgiji 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CROATIA YAWANG'OA WENYEJI URUSI KWA MATUTA, KUKUTANA NA ENGLAND NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top