• HABARI MPYA

    Thursday, July 12, 2018

    FEI TOTO ALIYETAMBULISHWA SINGIDA UNITED ASUBUHI, JIONI HII AIBUKIA YANGA NAKO KASAINI MIAKA MITATU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye mchana wa leo ametambulishwa na Singida United – jioni hii ametangazwa Yanga kwamba amejiunga na kwa mkataba wa miaka mitatu.
    Fei alikuwepo makao makuu ya klabu ya Yanga akiwa na jezi ya klabu huyo na kutambulishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika kama mchezaji mpya wa klabu hiyo pamoja na kiungo mwingine, Jaffar Mohammed kutoka Maji Maji ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.
    Feisal hakutaka kuzungumza chochote kuhusu kuonekana anatambulishwa na Singida United, lakini Meneja wa JKU, Mohammed Kombo aliyekuwapo mkutanoni pia amesema kwamba Yanga imekamilisha taratibu za kumchukua mchezaji huyo.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika (katikati) akiwa na wachezaji wapyam Feisal Salum (kushoto) na Jaffar Mohammed (kulia) 

    Feisal Salum (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika

    Mapema leo, Singida United imemtambulisha Fei Toto kwa kutoa picha akisaini mkataba na kukabidhiwa jezi ya timu hiyo. 
    Na katika taarifa yake, Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Zanzibar amesaini mkataba wa miaka mitatu.
    Sanga alisema kwamba Fei alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa JKU, lakini walizungumza na klabu yake na kufikia makubaliano ya kuununua mkataba huo. 
    Bado haijulikani nini kimejificha nyuma ya usajili wa Fei Toto – baada ya kuonekana anasaini Singida United asubuhi na jioni hii anaibukia Yanga.
    Lakini kwa mujibu wa kanuni za usajili, iwapo itagundulika Fei amesaini mikataba na timu zote, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufungiwa kuanzia mwaka mmoja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FEI TOTO ALIYETAMBULISHWA SINGIDA UNITED ASUBUHI, JIONI HII AIBUKIA YANGA NAKO KASAINI MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top