• HABARI MPYA

  Friday, July 13, 2018

  BEKI WA KATI JOB IBRAHIM WA NDANDA FC ALIYEWAHI KUCHEZEA YANGA SC ASAINI LIPULI FC

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa imeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao, baada ya kumsaini beki wa Ndanda FC ya Mtwara, Job Ibrahim.
  Job, mlinzi hodari wa katikati aliyewahi pia kuchezea Yanga SC, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na kikosi cha kocha Suleiman Abdallah Matola.
  Job anafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Lipuli FC kufika watano baada ya kiungo, William Lucian ‘Gallas’ kutoka Ndanda FC pia, washambuliaji Miraj Madenge ‘Shevchenko’ kutoka Mwadui FC, Paul John Nonga kutoka Mwadui FC ya Shinyanga ambao wote kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Issa Ally Rashid, mchezaji huru aliyesaini mkataba wa miaka miwili.
  Job Ibrahim (kushoto) wakati anasaini Lipuli FC jana mjini Iringa
    

  Gallas na Shevcheko wanakwenda kuungana tena na Suleiman Matola, aliyekuwa kocha wao kuanzia timu ya vijana ya Simba SC chini ya umri wa miaka 20, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na baadaye kuchwa mwaka 2014.
  Na Nonga anakwenda kukutana tena na mshambuliaji Malimi Busungu, ambaye walicheza naye Yanga SC miaka mitatu iliyopita chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kabla ya wote kuondoka kutokana na kutopata nafasi kikosi cha kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI WA KATI JOB IBRAHIM WA NDANDA FC ALIYEWAHI KUCHEZEA YANGA SC ASAINI LIPULI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top