• HABARI MPYA

  Wednesday, July 11, 2018

  AZAM FC YAIPIGA GOR MAHIA 2-0 NA KUTANGULIA FAINALI KOMBE LA KAGAME

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Azam FC sasa watasubiri mshindi kati ya Simba SC na JKU ya Zanzibar ikutane naye fainali Ijumaa hapa Taifa kujaribu kutetea taji lake ililolitwaa mwaka 2015 Dar eds Salaam pia.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani Azam FC ililazimika kusubiri hadi dakika 30 za nyongeza kupata tiketi ya kwenda fainali, baada ya kubanwa kwa sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Mabao ya Azam FC ambayo leo ilimkosa kinara wake wa mabao, Shaaban Iddi Chilunda yamefungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 92 na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa dakika ya 100.

  Ditram Nchimbi akipasua katikati ya wachezaji wa Gor Mahia leo Uwanja wa Taifa

  Jana CD Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania iliiandikia barua Azam FC kuizuia kumtumia Chilunda katika Kombe la Kagame ambaye hadi kufika hatua ya Robo Fainali alikuwa amekwishafunga mabao saba.
  CD Tenerife iliyomnunua kwa mkopo Chilunda wiki iliyopita baada ya kuvutiwa na mchezaji mwingine wa Tanzania, Farid Mussa kutoka akademi ya Azam pia - imesema inahofia mchezaji huyo anaweza kuumia kwenye mashindano ya Kagame.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA GOR MAHIA 2-0 NA KUTANGULIA FAINALI KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top