• HABARI MPYA

  Wednesday, June 13, 2018

  ZFA YAZIDI KUMOMONYOKA, MWINGINE NAYE ANG'ATUKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAKAMU wa Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA PEMBA) Ali Mohammed nae amejiuzulu rasmi nafasi yake kuongoza chama hicho.
  Akitoa sababu zilizopelekea kujiuzulu nafasi hiyo Mohammed amesema kutokana na viongozi wenzake wa juu kujiuzulu nae kaamua akae pembeni ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuliongoza soka la Zanzibar.
  Taarifa kama hiyo ni muendelezo ndani ya chama hicho kufutia viongozi wengine wajuu akiwemo akiwemo alokuwa Rais Ravia Idarous Faina pamoja na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali nao kujiuzulu siku chache zilizopita.
  Ali Mohammed nae amejiuzulu rasmi nafasi yake kuongoza chama hicho

  Inaonekana wazi chanzo cha viongozi wote hao kujiweka pembeni ni kuhusu uzembe uliofanywa kati yao na kupelekea timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana U-17 (Karume Boys) kuondolewa katika Mashindano ya CECAFA na kupigwa faini ya Dola elfu kumi na tano pamoja na kuzuiliwa kutoshiriki Mashindano yote yatakayoendeshwa na Baraza hilo mpaka kulipa kwa faini hiyo kwa kosa la kupeleka wachezaji wakubwa waliozaliwa chini ya tarehe 01/01/2002.
  April 19, 2018 ZFA ilizungumza na Vyombo vya Habari kupitia Makamo wake huyo (Ali Mohammed) na kukataa kuwa CECAFA hawajatuma ufafanuzi wa umri kwa wachezaji walotakiwa kushiriki mashindano ya CECAFA ya Vijana (U-17) yalofanyika Burundi mwaka huu huku ikimtupia lawama katibu wa CECAFA Nicholas Musonye.
  Lakini Mei 30, 2018 alokuwa Makamo wa Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali alikiri kupokea barua inayofafanua kuhusu umri wa wachezaji wanaotakiwa kushiriki katika mashindano hayo jambo ambalo likionekana yeye ndio nambari moja wa kulaumiwa mpaka mwenyewe akaamua kujiuzulu siku hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZFA YAZIDI KUMOMONYOKA, MWINGINE NAYE ANG'ATUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top