• HABARI MPYA

    Monday, June 04, 2018

    ZAMU YA SIMBA SC LEO NA KESHO SINGIDA UNITED SPORTPESA SUPER CUP

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC leo wanaingia Uwanja wa Nafraha mjini Nakuru, Kenya kumenyana na Kariobangi Sharks katika mchezo wake wa kwanza wa SportPesa Super Cup.
    Mchezo huo utafuatiwa na mchezo wa pili na wa mwisho wa hatua za awali kati ya wenyeji wengine, AFC Leopards dhidi ya Singida United kesho.
    Katika mechi za hizo, zote zinatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wapya zilizowasajili Kwa Simba miongoni kwa waliosajiliwa ni mshambuliaji kutoka Tanzania Prisons, Mohammed Abdallah na Singida United na mpachika mabao kutoka Mbao FC, Habib Kiyombo.
    Simba na Singida zitakwenda Uwanja wa Nafraha baada ya kuwashuhudia ndugu zao, Yanga na JKU kutoka Tanzania pia wakitupwa nje ya mashindano na timu za Kenya.

    Mshambuliaji mpya kutoka Tanzania Prisons, Mohammed Abdallah anaweza kucheza leo dhidi ya Kariobangi Sharks

    Ilianza Yanga SC kuchapwa 3-1 na Kakamega Homeboyz hapo hapo Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Allan Watende Wanga akifunga mabao mawili dakika za 26 na 30 na linguine la Kakamega Homeboyz likifungwa Wycliffe Opondo dakika ya 85, huku la timu ya Jangwani mjini Dar es Salaam likifungwa na Matheo Anthony dakika ya 38.
    JKU nayo ikafuatia baada ya kuchapwa 3-0 na mabingwa watetezi, Gor Mahia mabao ya George Odhiambo, Godfrey Walusimbi na Meddie Kagere na sasa wanapanda ndege moja na ndugu zao, Yanga SC kurejea Dar es Salaam kila timu ikipatiwa kifuta jasho cha dola za Kimarekani 2,500 kiasi cha Sh. Milioni 6.
    Kakamega Homeboys sasa watakutana na Gor Mahia katika Nusu Fainali Juni 7, na Nusu Fainali ya pili itakutanisha washindi wa mechi za leo.
    Na fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Juni 10 na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
    Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMU YA SIMBA SC LEO NA KESHO SINGIDA UNITED SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top