• HABARI MPYA

  Sunday, June 03, 2018

  YANGA SC ‘WAKOKOMEKWA’ 3-1 NA KAKAMEGA HOMEBOYZ NA KUTUPWA NJE SPORTPESA SUPER CUP

  Na Mwandishi Wetu, NAKURU
  YANGA SC imeendelea kuogelea kwenye wimbi la matokeo mabaya, baada ya kutolewa hatua hatua ya kwanza tu ya michuano ya SportPesa Super Cup kufuatia kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Kakamega Homeboyz Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
  Kikosi cha Yanga SC kilichofungwa 3-1 leo na Kakamega Homeboyz leo


  REKODI YA YANGA SC TANGU AONDOKE LWANDAMINA  

  Aprili 11, 2018; Yanga 1-1 Singida United (Ligi Kuu Dar es Salaam)

  Aprili 18, 2018; Welayta Dicha 1-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho)

  Aprili 22, 2018; Mbeya City 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya)

  Aprili 29, 2018; Simba 1 – 0 Yanga SC (Ligi Kuu Dar es Salaam)

  Mei 6, 2018; USM Alger 4-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho Algiers)

  Mei 10, 2018; Tanzania Prisons 2-0 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya)

  Mei 13; 2018; Mtibwa Sugar 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu Morogoro)

  Mei 16, 2018; Yanga SC 0-0 Rayon Sports (Kombe la Shirikisho Dar es Salaam)

  Mei 19, 2018; Yanga SC 0-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)

  Mei 22, 2018; Yanga SC 1-0 Mbao FC (Ligi Kuu Dar es Salaam)

  Mei 25, 2018; Yanga SC 2-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Dar es Salaam)

  Mei 28, 2018; Yanga SC 1-3 Azam FC (Ligi Kuu Dar es Salaam)

  Juni 3, 2018; Yanga SC 1-3 Kakamega Homeboys (SportPesa Super Cup)


  Hicho kinakuwa kipigo cha saba katika mechi 14, nyingine saba ikitoa sare sita na kushinda moja tangu kuondokewa na aliyekuwa kocha Mkuu wake, Mzambia George Lwandamina.
  Japokuwa tayari imeleta kocha Mkuu mpya, Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyesaini mkataba wa miaka miwili mwezi uliopita, lakini Yanga imeendelea kuongozwa na waliokuwa makocha Wasaidizi wa Lwandamina, Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Kakamega Homeboyz yamwefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Allamn Watende Wanga mawili dakika za 26 na 30 na Wycliffe Opondo dakika ya 85, wakati bao pekee la Yanga limefungwa na Matheo Anthony dakika ya 38.
  Mchezo wa pili unaendelea sasa mabingwa watetezi, Gor Mahia wakimenyana na JKU ya Zanzibar, wakati Simba SC watatupa mguu wao wa kwanza kesho kwa kumenyana na Kariobangi Sharks katika mchezo wa mchana, kabla ya Singida United kumenyana na AFC Leopards jioni.
  Washindi wa mechi hizo watakutana katika Nusu Fainali Juni 7, ya kwanza ikikutanisha washindi wa mechi za leo na ya pili ikikutanisha washindi wa mechi za kesho.
  Na fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Juni 10 na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
  Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC ‘WAKOKOMEKWA’ 3-1 NA KAKAMEGA HOMEBOYZ NA KUTUPWA NJE SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top