• HABARI MPYA

    Monday, June 11, 2018

    WALIOIPA UFARANSA KOMBE LA DUNIA 1998 WAKUTANA KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA USHINDI WAO

    WACHEZAJI wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 leo Jumatatu wameungana ikiwa ni miaka 20 tangu waifunge 3-0 Brazil na kutwaa taji hilo.
    Christian Karembeu, Fabien Barthez, Lionel Charbonnier, Robert Pires, Zinedine Zidane, Youri Djorkaeff, Vincent Candela, Alain Boghossian, Laurent Blanc na Sabri Lamouchi wote walihudhuria tukio hilo mjini Saint-Denis kusherehekea miaka 20 ya ushindi huo.
    Mabao mawili ya Zidane na moja la Emmanuel Petit yalitosha kuipa Ufaransa ushindi mnono dhidi ya Brazil Uwanja wa Stade de France mjini Saint-Denis. 

    Wachezaji walioipa Ufaransa Kombe la Dunia mwaka 1998 leo wameungana kusherehekea miaka 20 tangu waifunge 3-0 Brazil na kutwaa taji hilo 
    Wachezaji hao wa zamani walipiga picha za pamoja na nyingine wakipiga na watoto wa eneo hilo la mji wa Paris, wakati kocha wa zamani wa Real Madrid, Zidane alikamata kipaza sauti na kuongoza sherehe. 
    Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwepo kwneuye fainali ya michuano ya tenisi ya French Open Jumapili akishuhudia Rafael Nadal akimfunga Dominic Thiem.
    Nyota wa zamani wa Monaco, Paris Saint-Germain na Inter Milan, Djorkaeff, ambaye pia alichezea Bolton na Blackburn pia alikuwepo kwenye fainali Roland-Garros.
    Gwiji wa zamani wa Arsenal, Pires alikuwepo nchini Ufaransa baada ya kukichezea kikosi cha Dunia XI dhidi ya England katika Soccer Aid Uwanja wa Old Trafford Jumapili usiku. 
    Wakati huo huo; Kikosi cha Didier Deschamps kimeendelea na maandalizi ya Kombe la Dunia kwa mazoezi makali Jumatatu ya leo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WALIOIPA UFARANSA KOMBE LA DUNIA 1998 WAKUTANA KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA USHINDI WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top