• HABARI MPYA

  Monday, June 04, 2018

  TFF YAFURAHISHWA NA FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeridhishwa na maandalizi yaliyofanikisha mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) ikiwa pamoja na kuwashukuru Wadau mbalimbali.
  Fainali hiyo iliyowakutanisha Mtibwa Sugar na Singida United ilikuwa ya aina yake kwa ushirikiano wa TFF na Wadau mbalimbali.
  "TFF inachukua nafasi hii kuishikuru Serikali ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Mrisho Gambo kwa kuwa sehemu ya kufanikisha Fainali hiyo,". 
  "TFF inamshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndugu Athuman Kihamia, Wananchi wa Arusha na mashabiki waliosafiri kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya jirani kushuhudia mchezo huo wa Fainali,".

  Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha Jumamosi

   Aidha, TFF pia imetoa shukrani za dhati kwa Azam Tv Wadhamini wakuu wa Azam Sports Federation Cup kwa msimu wa tatu sasa na pia tunatoa shukrani kwa wadhamini waliojitokeza kwenye mchezo wa Fainali Benki ya KCB.
  Kwenye mchezo huo wa Fainali Mtibwa Sugar walifanikiwa kutwaa taji jilo baada ya kuifunga Singida United kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.
  Mtibwa Sugar wamezawadiwa medali,fedha shilingi milioni 50 na Kombe wakati Singida United kwa kumaliza nafasi ya pili wamepata medali na fedha shilingi milioni 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAFURAHISHWA NA FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top