• HABARI MPYA

    Saturday, June 09, 2018

    TFF WAACHANE NA YANGA, WAICHUKUE SINGIDA UNITED KAMA LENGO NI TANZANIA IFANYE VIZURI KOMBE KA KAGAME

    Na Winchislaus Josephath
    NIMEKUWA msomaji wa makala zako to unaandika kwenye blog hadi leo hii kwenye website. Shida tu ni moja kwamba website yako hairuhusu comments kwenye makala zako. 
    Ila nikupongeze kwamba mara zote umekuwa ukisimamia ukweli.
    Nia yangu leo ni kujaribu kuhoji juu ya nafasi ya TFF tuliyonayo sasa kusaidia vilabu vya nyumbani kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki.
    Kwa mfano, najiuliza TFF wana malengo gani na michuano ya Kagame? wanapeleka timu ili zikashiriki au tunapeleka timu zikashindane? Yanga wamejitathmini na wamegundua hawana timu ya kushindana, unawezaje kuwalazimisha washiriki? au timu inavyofungwa na kutia aibu, TFF wanafaidika na nini? 

    Kila mtu anajua kuwa wachezaji Yanga hawajalipwa mishahara wala posho zao kwa kipindi kirefu. Kila mtu anajua kuwa Yanga hata Ligi wamemaliza kwa kubahatisha hadi wanakula kwa mama ntilie kwa kukOsa hela za maandalizi.
    Kila mtu anajua kuwa sasa hivi Yanga haina kocha maana, Nsajigwa vyeti vyake havimruhusu kukaa benchi kama kocha mkuu hata kwenye VPL.
    Wachezaji wengi wamegoma na timu imebaki na kikosi kidogo tena kisicho na ubora. Wakati timu inajipanga ili iweze kurekebisha makosa kwa ajili ya michuano ya CAF; TFF inawalazimisha eti wakashiriki Kagame na si kushindana. 
    Ndo hapo najiuliza hii TFF haiyaoni haya? au wanafaidika na nini kuona Yanga inafanya vibaya? Mbona kuna timu nyingi nzuri zenye uwezo wa kushindana? 
    Kwa nini wasizipeleke hizo? Binafsi naamini Simba, Azam, Singida United, Mtibwa Sugar ni bora kuliko Yanga ya sasa. Ni aibu kuona kiongozi wa TFF anailinganisha Yanga na Gor Mahia, Rayon eti kwa sababu zote zinashiriki CAF bila kuangalia ni katika mazingira yapi. 
    Pia lazima kujua kuwa Wakenya ni Wakenya, Wanyarwanda ni Wanyarwanda, na Watanzania ni Watanzania. TFF haiwezi kupata sifa eti kwa sababu Gor Mahia au Rayon wamefanya vizuri kwenye mashindano. 
    Ni Yanga pekee anaweza kuwaletea sifa tena na nafasi ya kuongeza timu kwenye mashindano ya CAF iwapo watafanya vizuri. 
    Na si Yanga pekee ambao wamefanya hivyo, Sudan wamewahi kujitoa kwa kigezo hicho hicho na bado haikuwa shida.
    Ni wakati TFF iangalie maendeleo ya soka letu badala ya kuangalia mapato.
    (Kama alivyojitambulisha, mwandishi wa makala hii, Winchislaus Josephath ni msomaji wa muda mrefu wa Bin Zubeiry Sports - Online) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF WAACHANE NA YANGA, WAICHUKUE SINGIDA UNITED KAMA LENGO NI TANZANIA IFANYE VIZURI KOMBE KA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top