• HABARI MPYA

    Thursday, June 07, 2018

    SIMBA YATINGA FAINALI SPORTPESA SUPER CUP KWA PENALTI 5-4 BAADA YA SARE YA 0-0 TENA

    Na Mwandishi Wetu, NAKURU
    SIMBA SC imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
    Waliofunga penalti za Simba SC leo ni viungo, Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomary Kapmbe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude, wakati Gor Mahia walipiga juu penalti yao ya mwisho.
    Simba SC sasa itakutana na mshindi wa mchezo unaoendelea sasa kati ya mabingwa watetezi, Gor Mahia na Singida United ya Tanzania katika fainali Jumapili.
    Kikosi cha Simba SC kilichoanza katika mchezo wa leo Uwanja wa Afraha mjini Nakuru  

    Ikumbukwe mchezo wa kwanza pia Simba ilipenya kwa matuta, ikishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya nayo, kabla ya kuendeleza ushindi wa staili hiyo mbele ya Kakamega iliyowatoa Yanga  ya Tanzania pia kwa kuwachapa 3-1.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YATINGA FAINALI SPORTPESA SUPER CUP KWA PENALTI 5-4 BAADA YA SARE YA 0-0 TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top