• HABARI MPYA

    Sunday, June 17, 2018

    SIMBA NA PRISONS ROBO FAINALI YA ‘KUFA MTU’ KOMBE LA UHAI LEO

    Na Mwandishi Wetu, DODOMA
    HATUA ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo kwa mechi mbili kupigwa viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
    Mabingwa watetezi, Simba SC wanateremka uwanjani kumenyana na Tanzania Prisons, mchezo ambao utatanguliwa na mechi nyingine ya Robo Fainali, kati ya Stand United na Ndanda FC.

    Na hiyo ni baada ya Robo Fainali mbili za kwanza kufanyika jana, ikishuhudiwa Azam FC na Mtibwa Sugar zikitangulia Nusu Fainali kwa ushindi wa 1-0 kila timu. Azam FC iliifunga Mbao FC, bao pekee la Paul Peter dakika ya 60 na Mtibwa Sugar iliifunga Ruvu Shooting bao pekee la Abuu Juma dakika ya 55.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA PRISONS ROBO FAINALI YA ‘KUFA MTU’ KOMBE LA UHAI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top