• HABARI MPYA

  Sunday, June 10, 2018

  SIMBA B YAANZA VYEMA KOMBE LA UHAI, PRISONS, NDANDA, STAND NAZO ZASHINDA UDOM

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza vyema michuano ya Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ushidi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida United.
  Ushindi huo katika mchezo huo wa Kundi B umetokana na mabao ya Meshack Abel dakika ya 19 na Modest Matinyange dakika ya 78, wakati bao pekee la Singida limefungwa na Said Habib dakika ya 90.
  Mechi nyingine ya Kundi B leo, Stand United imeichapa Njombe Mji FC 1-0, bao pekee la Frank Zakaria dakika ya 88.

  Mechi nyingine mbili za Kundi D leo, Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Lipuli FC mabao ya Abubakar Maulika dakika ya 43 na Ramadhan Ibata dakika ya 66, wakati Ndanda FC imeilaza 2-1 Kagera Sugar, mabao ya washindi yakifungwa na Juma Said Athumani dakika ya 42 na Yassin Hamad Rashid dakika ya 60 dhdii ya la Haroun Ally Said dakika ya 88.
  Michuano hiyo itaendelea kesho mechi za Kundi A kati ya Mbao FC na Yanga, Saa 8:00 mchana na Ruvu Shootong na Mbeya City Saa 10:00 jioni na za Kundi C Mtibwa Sugar na Mwadui FC Saa 8:00 mchana na Maji Maji dhidi ya Azam FC Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA B YAANZA VYEMA KOMBE LA UHAI, PRISONS, NDANDA, STAND NAZO ZASHINDA UDOM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top