• HABARI MPYA

  Monday, June 04, 2018

  NGOMA AWASILI SALAMA AFRIKA KUSINI, KUFANYIWA VIPIMO LEO

  Na Saada Salmin, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC, Mzimbabwe Donald Ngoma amewasili salama mjini Cape Town, Afrika Kusini tayari kufanyiwa vipimo.
  Ngoma aliondoka jana Saa 3:45 usiku akiongozana na Daktari Mkuu wa klabu, Mwanandi Mwankemwa kwenda Capetown ambako leo atafanyiwa vipimo vya maumivu yaliyomuweka nje kwa msimu mzima akiwa Yanga kama amepona.
  Dk Mwankemwa amesema kwamba wamefika salama na kwa sasa wanajiandaa kwenda hospitali kwa ajili ya kuanza vipimo.

  Donald Ngoma (kulia) akiwa na Daktari Mkuu wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa wakati wa safari yao jana

  Kwa mujibu wa makubaliano ya mchezaji huyo wa zamani wa FC Platunums ya Zimbabwe na klabu hiyo ya Aljah Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake – majibu ya vipimo hivyo ndiyo yataamua mustakabali wake Azam FC.
  Wakati inamchukua kutoka Yanga mwezi uliopita, Azam ilisema kwamba Ngoma atasaini mkataba rasmi baada ya vipimo vya Afrika Kusini kama vitaonyesha amepona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOMA AWASILI SALAMA AFRIKA KUSINI, KUFANYIWA VIPIMO LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top