• HABARI MPYA

  Friday, June 15, 2018

  NEYMAR: NINGEKUWEPO UJERUMANI WASINGETUPIGA SABA

  NYOTA wa Brazil, Neymar amesema kama angekuwepo uwanjani katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014, basi Brazil isingefungwa mabao 7-1 na Ujerumani.
  Neymar hakucheza mechi hiyo ya fainali kutokana na majeraha ya mgongo aliyoyapata katika fainali hizo zilizofanyika Brazil na Ujerumani kutwaa ubingwa.
  "Nilipenda kucheza mchezo ule lakini hali haikuweza kuniruhusu, na naamini tusingefungwa mabao yote yale na natamani mechi ile ijirudie tena.
  Neymar amesema kama angekuwepo uwanjani katika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil isingefungwa mabao 7-1 na Ujerumani

  “Yaani niwe uwanjani naichezea Brazil halafu tufungwe mabao yote hayo? Haiwezekani naamini kama ningecheza mechi ile matokeo yangekuwa tofauti kabisa," amesema Neymar.
  Neymar alikosa kucheza mechi ya nusu fainali kwenye Uwanja wa Belo Horizonte baada ya kuumia katika robo fainali dhidi ya Colombia.
  Katika fainali za Kombe la Dunia za 21 zilizoanza leo huko Urusi, Neymar anayechezea Brazil ndiye mchezaji ghali zaidi akiwa na thamani ya dola milioni 261.
  PSG ilimnunua Neymar kutoka Barcelona kwa dau la dola milioni 261 na kuweka rekodi ya dunia ya usajili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR: NINGEKUWEPO UJERUMANI WASINGETUPIGA SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top