• HABARI MPYA

  Monday, June 11, 2018

  MTIBWA SUGAR ‘YAFUNGULIA MBWA’ KOMBE LA UHAI, YANGA NA AZAM BADO ZASUASUA

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 3-1 Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa Kundi C viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya Omar Sultan dakika ya 20, Richard Mwamba dakika ya 26 na Onesmo Justin dakika ya 28 dhidi ya moja la Frank Mushi dakika ya 85, Mtibwa Sugar inafikisha pointi nne baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Azam FC ya Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza.

  Mtibwa Sugar imepata ushindi wa kwanza katika Kombe la Uhai 

  Mechi nyingine ya Kundi C leo, Azam FC imelazimishwa sare nyingine ya 0-0 na Maji Maji ya Songea, wakati mechi za Kundi A, Yanga nayo imetoa sare ya pili mfululizo ya 0-0, safari hii na Mbao FC, wakati bao pekee la Abdallah Mgemwa dakika ya 21 limetosha kuipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR ‘YAFUNGULIA MBWA’ KOMBE LA UHAI, YANGA NA AZAM BADO ZASUASUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top