• HABARI MPYA

  Monday, June 11, 2018

  MECHI ZOTE SASA 'LIVE' KIGANJANI MWAKO KUPITIA TIGO 4G

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MASHABIKI wa soka nchi nzima wana sababu ya kushangilia kufuatia ushirikiano mkubwa kati ya Tigo Tanzania na StarTimes.
  Tigo- mtandao unaoongoza kwa huduma bora za kidigitali, pamoja na mrushaji rasmi wa Kombe la Dunia - Star Times wameungana kuwawezesha Watanzania kutazama laivu kwenye simu zao za mkononi mechi zote za tukio kubwa zaidi la mpira wa miguu kwa mwaka 2018. 
  Kama tunavyojua tukio hili kubwa zaidi la soka litakalofanyika Urusi kuanzia wiki hii ndio tukio linalotazamwa zaidi duniani.
  Mkuu wa Idara ya Masoko ya Tigo, William Mpinga (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari leo ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Slipway, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo. Kulia ni Meneja Masoko StarTime, David Malisa  
  Mkuu wa Idara ya Masoko ya Tigo, William Mpinga akibadilishana na mipira na Meneja Masoko StarTime, David Malisa  
  Afisa Uhusiano wa StarTime, Samuel Gisayi akitoa maelekezo ya matumizi ya Application hiyo

  Tigo inajivunia kwa mara ya kwanza kabisa, kuwaletea mashabiki wa soka  maajabu ya tukio hili kubwa zaidi la soka moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi. Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bunifu zinazoboresha maisha yao ya kidigitali. 
  Ili kuhakikisha kuwa mashabiki wa soka wanafurahia msimu huu wa soka,  Tigo imeungana na mrushaji rasmi wa Kombe la Dunia, StarTimes kuzindua StarTimes Application.
  Star times Application itawezesha wapenzi wote wa soka kuwa sehemu ya msisimko, furaha na huzuni yanayoendana na tukio hili linalotazamwa zaidi duniani kupitia mtandao mpana zaidi wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 22 nchini.
  Hakuna shabiki aliye na kisingizio cha kukosa mechi, magoli, na mada zote zinazoendana na tukio hili kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018. 
  Yeyote, popote nchini Tanzania sasa anaweza kutazama mechi zote laivu kwenye simu janja ya mkononi kwa kupakua application ya StarTimes App na kununua bando ya intaneti kutoka menu ya Tigo iliyoboreshwa ya *147*00#. Watanzania wanaweza kuchagua bando za saa, siku, wiki au mwezi kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#. 
  Kisha wataweza kutazama mechi zote 64 za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 moja kwa moja kwenye simu zao janja wakiwa popote nchini huku wakifurahia ubora wa hali ya juu wa huduma za intaneti za Tigo 4G, mtandao mpana, wenye kasi ya juu na wa uhakika zaidi nchini. 
  Hali kadhalika, mashabiki wanaweza kutazama mechi laivu na kupata habari za uhakika za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 kupitia Tigo Sports Portal  www.tigosports.co.tz  au kwa kujiunga kupitia menu ya Tigo iliyoboreshwa ya *147*00#. 
  Tigo Sports Portal ndio kituo cha kidigitali chenye habari za kusisimua za tukio hili kubwa zaidi la kisoka.
  Kupitia Tigo Sports portal mashabiki pia wanaweza kushiriki kujibu maswali yanayohusu dondoo za soka na kushinda zawadi nono hadi TSH 10 milioni kupitia shindano la SMS. 
  Kwa mara nyingine, Tigo inajivunia kwa mara ya kwanza kabisa, kuwaletea mashabiki wa soka  maajabu ya tukio hili kubwa zaidi la soka moja kwa moja kwenye simu zao za mkononi. 
  Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja wake na kuwapa bidhaa na huduma bunifu zinazoboresha maisha yao ya kidigitali. 
  Tunawakaribisha mashabiki wote wafurahie msimu huu mkubwa zaidi wa soka kwa  mwaka 2018 kwa kupakua Startimes App, kununua bando kupitia *147*00# na kujiunga na Tigo Sports Portal  ili waweze kutazama mechi zote laivu, wapate dondoo muhimu za soka pamoja na kupata nafasi ya kushinda zawadi murwa hadi TSH 5 milioni kutoka Tigo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI ZOTE SASA 'LIVE' KIGANJANI MWAKO KUPITIA TIGO 4G Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top