• HABARI MPYA

    Wednesday, June 06, 2018

    MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS, AFRICAN SPORTS AFARIKI DUNIA TANGA, BITEBO 'ZEMBWELA' AFIWA NA MKEWE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Rajabu Digongwa aliyefariki mkoani Tanga. 
    Karia amesema kwamba amepokea kwa huzuni na mshituko mkubwa taarifa za kifo cha mchezaji huyo wa zamani aliyefariki dunai jana baada ya kuugua. 
    Karia ametoa pole kwa familia ya mchezaji huyo, wanafamilia wa mpira wa miguu, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu.
    “Marehemu Digongwa namfahamu vizuri toka enzi akicheza na kifo chake kimenishitua na kunihuzunisha, kwa niaba ya TFF natoa pole kwa wafiwa" alisema Karia. 

    Mshambuliaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Khalid Bitebo 'Zembwela' amefiwa na mkewe 

    Enzi za uhai wake marehemu Digongwa alicheza timu za Wananchi FC, African Sports, pia alipata kuitwa kwenye timu ya mkoa wa Tanga na pia timu ya Taifa ya Tanzania.
    Mazishi ya marehemu Digongwa yamefanyika leo majira ya saa 4 asubuhi mkoani Tanga 
    Wakati huo huo: Rais Karia pia ametuma salamu za rambirambi kwa mshambuliaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Khalid Bitebo 'Zembwela' aliyefiwa na mkewe. 
    Ametoa pole kwa Bitebo na familia kiujumla akiwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS, AFRICAN SPORTS AFARIKI DUNIA TANGA, BITEBO 'ZEMBWELA' AFIWA NA MKEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top