• HABARI MPYA

  Tuesday, June 05, 2018

  MASOUD JUMA AKATAA KUONDOKA SIMBA SC HADI AFUKUZWE NA YEYE

  Na Mwandishi Wetu, NAKURU
  KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Mrundi Irambona Masoud Juma amesema kwamba anaridhika na nafasi yake na anachopata katika klabu hiyo na hana mpango wa kuondoka labda afukuzwe.
  Juma, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Burundi ameyasema hayo mjini Nakuru, Kenya kufuatia kuibuka kwa uvumi wa kwamba amejiuzulu.
  “Mimi nina mkataba Simba. Mimi nimekuja kutoka nyumbani kuja kufanyia kazi Simba, sina mawazo leo au kesho kusema eti nijiuzulu, labda wenyewe wanifukuze,”amesema Juma leo mjini Nakuru, ambako Simba ipo kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.

  Mrundi Masoud Juma (kushoto) amesema kwamba anaridhika na anachokipata Simba

  Juma alikuja nchini Oktoba mwaka jana na kuanza kazi kama Msaidizi wa Joseph Marius Omog hadi Desemba alipokaimu Ukocha Mkuu kufuatia Mcameroon huyo kufukuzwa.
  Masoud Juma alikaimu Ukocha Mkuu Simba SC hadi Janauri alipowasili Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye aliambatana na Msaidizi wake mmoja, Mtunisia Aymen Mohammed Hbibi.
  Na Juma akiwa Msaidizi wa Omog aliiongoza Simba katika mechi 10, ikishinda sita, sare nne ikiwemo waliyomalizia kwa kufungwa kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 katika hatua ya 64 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federatiuon Cup (ASFC) Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Na akiwa Kaimu kocha Mkuu, Simba ilicheza mechi saba ikishinda nne, sare moja na kufungwa mbili, wakati akiwa Msaidizi wa Lechantre Simba imecheza mechi 22 hadi sasa, ikishinda 14, sare saba na kufungwa moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASOUD JUMA AKATAA KUONDOKA SIMBA SC HADI AFUKUZWE NA YEYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top