• HABARI MPYA

  Wednesday, June 06, 2018

  MAN UNITED YASAJILI BEKI KIJANA MDOGO WA MIAKA 19

  KLABU ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki wa pembeni, Diogo Dalot kutoka FC Porto kwa mkataba wa miaka mitano.
  Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya vijana ya Ureno chini ya umri wa miaka 21 amejiunga na klabu hiyo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 17.4 wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja. 
  United inataka beki wa kulia wa kwenda kushindana na mkongwe, Antonio Valencia, ambaye akiwa na umri wa miaka 33 na anasumbuliwa na maumivu ya goti, hivyo anahitaji matibabu ya uhakika. 

  Beki wa kulia, Diogo Dalot amesaini Manchester United kwa dau la Pauni Milioni 17 kutoka Porto 

  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, anaweza pia kucheza kama beki wa kushoto. 
  Aliibukia kwenye kikosi cha kwanza cha Porto mwezi Februari akicheza nafasi hiyo katika sare ya 0-0 na Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa.
  Aliisaidia Ureno kushinda Kombe la Mataifa ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, akifunga mabao mawili katika mechi tano mjini Azerbaijan, likiwemo moja la kwenye fainali dhidi ya Hispania. 
  Juu ya usajili wa kinda huyo, kocha wa United, Jose Mourinho ameiambia tovuti ya klabu tovuti rasmi ya klabu: "Diogo ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, beki kijana mdogo na mwenye ubora wa kuwa mchezaji mkubwa haraka katika klabu hii,". 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YASAJILI BEKI KIJANA MDOGO WA MIAKA 19 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top