• HABARI MPYA

    Thursday, June 14, 2018

    LOPETEGUI AONDOKA URUSI KWA AIBU, ATUA MADRID KIFALME

    KOCHA Julen Lopetegui ameondoka Urusi kufuatia kufukuzwa timu ya Hispania siku mbili kabla ya fainali za Kombe la Dunia.
    Lopetegui alifukuzwa jana Hispania kufuatia kutangazwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid akiwa maandalizi ya mwisho ya Kombe la Dunia.
    Na usiku wa jana, kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 alipigwa picha akipakia mizigo yake kwa safari ya Uwanja wa Ndege wa Krasnodar kurejea Hispania.
    Julen Lopetegui akiwa na mabeki yake baada ya kuondoka Urusi 
    Taarifa zinasema mchana wa leo Alhamisi, Lopetegui angeweza kutambulishwa kama kocha mkuu wa Madrid kwenye uwanja wa timu hiyo wa Santiago Bernabeu. 
    Akizungumza kabla ya kuondoka jijini Krasnodar, huko Urusi, Lopetegui amesema. "Imeniuma sana, lakini nawatakia Hispania mafanikio mema katika Kombe la Dunia ikiwezekana kutwaa ubingwa," amesema Lopetegui akiwa katika uso unaomaanisha kile asemacho. "
    Miongoni mwa changamoto zinazomkabiri Lopetegui kwa sasa katika kibarua chake kipya ni majaliwa ya nyota kadhaa wa Madrid ambao baadhi yao ni Cristiano Ronaldo, Odriozola, Alisson, na Gareth Bale.
    Tayari kocha mpya wa Hispania, Fernando Hierro ameanza kazi na kusema ana matumaini ya kufanya vizuri huku akisisitiza kutofanya mabadiliko yoyote yale kikosini.
    Hierro ambaye ni nyota wa zamani wa Klabu ya Real Madrid amepewa kazi ya kuinoa Hispania baada ya Kocha Julen Lopetegui kutimuliwa katika nafasi hiyo kutokana na kitendo chake cha kutangazwa kuwa kocha mpya wa Madrid.
    Hispania ipo Kundi B katika fainali za Kombe la Dunia zinazoanza leo saa 12:00 jioni na itacheza mechi yake ya kwanza Ijumaa wiki hii dhidi ya Ureno.
     “Ni wakati wangu mzuri wa kuwajibika na kuwathibitishia walionipa majukumu, kwa mazingira yalivyo sitafanya mabadiliko yoyote yale na niwatake mashabiki wetu kutoamisha matarajio yao, tutafanya vizuri,” amesema Hierro.
    Jumanne wiki hii Madrid ilimtangaza Lopetegui kuwa kocha wake mpya akichukua mikoba ya Zinedine Zidane huku akielezwa kuanza kazi baada ya Kombe la Dunia, lakini Shirikisho la Soka la Hispania kupitia kwa rais wake, Luis Rubiales liliamua kumfuta kazi kwani hakuwa amewaeleza lolote kuhusu mpango wake huo wa kwenda Madrid.
    Licha ya baadhi ya wachezaji wakongwe wa kikosi cha Hispania kushauri kocha huyo kutotimuliwa, Rubiales alimtimua na kumtangaza Hierro kuwa kocha moya kutoka katika nafasi ya mkurugenzi wa ufundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LOPETEGUI AONDOKA URUSI KWA AIBU, ATUA MADRID KIFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top