• HABARI MPYA

  Thursday, June 14, 2018

  LIPULI FC YAUNDA KAMATI YA USAJILI KUTAFUTA WAKALI WA KUENDELEZA MOTO MSIMU UJAO LIGI KUU

  Na Ibada Mkomwa, IRINGA
  KLABU ya Lipuli ya Iringa imepania kufanya usajili mzuri ili msimu ujao iendelee kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Hayo yamefikiwa katika kikao Kamati ya Utendaji ya Lipuli iliyocheza Ligi Kuu msimu huu baada ya muda mrefu tangu ishuke kilichofanyika juzi kujadili mambo mbalimbali likiwemo Suala la Usajili. 
  Mwenyekiti wa Lipuli FC, Ramadhan Mahano amesema kwamba kwa sasa wanasubiri kalenda ya TFF itolewe na kutangazwa na baada ya hapo watafanya usajili wa nguvu. 
  Mwenyekiti huyo pia amewahakikisha wanachama na wapenzi wa Lipuli kwamba Kamati ya Utendaji intafanya jitihada kumbakiza Kocha wake mmoja, Suleiman Matola baada ya kocha mwingine, Amri Said kutimkia Mbao FC.
  Amesema pia kikao cha juzi kimeunda Kamati ya Usajili ambayo itakuwa na kazi kubwa mbili ikiwa ni pamoja na kufanya usajili wa Wachezaji kwa Musimu wa 2018/2019 pia itakuwa na kazi ya kuhakikisha inapata fedha kwa ajili ya Usajili huo. 
  Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Ayoub Kihwelo na Wajumbe wake ni Ally Ngallah, Lonjino Malambo,  Evaristor Myovela, Dk. Bukaza Chachage, Nassoro Masangula, Sylivester Kanyika na Edgar Kifyoga na hivi karibuni itakutana mara moja ili kuanza majukumu yake.
  Amesema pia kwamba Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu ya Lipuli utafanyika Juni 30, mwaka huu kama ilivyopangwa katika ukumbi wa utatangazwa hivi karibuni.
  Moja ya ajenda za Mkutano huo ni kujaza nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji iliyowazi, hivyo Mahano amewaomba wanachama kujitokeza kugombea nafasi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIPULI FC YAUNDA KAMATI YA USAJILI KUTAFUTA WAKALI WA KUENDELEZA MOTO MSIMU UJAO LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top