• HABARI MPYA

  Thursday, June 07, 2018

  LIGI YA VIJANA YA TAIFA U-20 KUANZA KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI UDOM, INADHAMINIWA NA AZAM TV

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 inatarajiwa kuanza Jumamosi wiki hii viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ikishirikisha vikosi vya pili vya timu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita chini ya udhamini wa Azam TV.
  Upangaji wa ratiba na makundi ya Ligi ya Vijana U20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefanyika leo makao makuu ya Azam TV, Tabata mjini Dar es Salaam.
  Kundi A linaundwa na timu za Yanga SC, Ruvu Shooting, Mbeya City na Mbao FC, Kundi B kuna Simba, Singida United, Stand United na Njombe Mji, Kundi C kuna Azam FC, Mtibwa Sugar, Mwadui FC na Majimaji FC na Kundi D linaundwa na Tanzania Prisons, Lipuli FC, Kagera Sugar na Ndanda FC.

  Aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto), akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi ya U-20 Nahodha wa Simba U20, Moses Kitundu mwaka jana

  Katika kundi A Yanga SC watafungua pazia la mashindano hayo dhidi ya Ruvu Shooting saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili Mbeya City dhidi ya Mbao FC Juni 9,2018 saa 10 jioni.
  Mechi nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya kwanza ni za kundi C ambapo Azam FC watacheza na Mtibwa Sugar saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili utakaoanza saa 10 kati ya Mwadui na Majimaji 
  Kundi B wenyewe wataanza mechi zao Juni 10,2018 ambapo mabingwa watetezi, Simba watacheza dhidi ya Singida United nao Stand United watacheza na Njombe Mji saa 10 jioni.
  Mechi nyingine za siku hiyo ni za Kundi D Tanzania Prisons dhidi ya Lipuli FC saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Ndanda FC saa 10 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI YA VIJANA YA TAIFA U-20 KUANZA KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI UDOM, INADHAMINIWA NA AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top