• HABARI MPYA

  Friday, June 08, 2018

  LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE KUENDELEA WIKIENDI HII

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya nane bora inatarajia kuendelea Jumamosi Juni 9, mwaka huu, kufuaaia kusimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars na baadaye timu ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens.
  Viwanja vitatu ndivyo vitatumika kwa michezo hiyo ya wikiendi hii huku Uwanja wa Karume ukitumika kwa michezo miwili itakayochezwa saa 8 mchana na saa 10 jioni.
  Mechi hizo ni kati ya Evegreen vs Panama (Karume), Alliance vs JKT Queens (Nyamagana), Mlandizi Queens vs Baobab (Mabatini) na Simba Queens vs Kigoma Sisters (Karume).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE KUENDELEA WIKIENDI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top