• HABARI MPYA

  Thursday, June 14, 2018

  KIPYENGA CHA KWANZA CHAPULIZWA LEO KOMBE LA DUNIA 2018

  FAINALI za Kombe la Dunia zinatarajiwa kuanza leo kwa mchezo wa ufunguzi wa Kundi A, kati ya wenyeji, Urusi na Saudi Arabia kuanzia Saa 12:00 jioni Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow.
  Refa Nestor Pitana raia wa Argentina ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Juan Pablo Bellati na Hernan Maidana, huku Sandro Ricci raia wa Brazil akiwa mwamuzi mwamuzi wa akiba.
  Katika nafasi ya mwamuzi wa video anayetumia teknolojia ya ‘Video Assistant Referee (VAR)’ watakuwepo Massimiliano Irrati wa Italia (VAR) ambaye wasaidizi wake ni Mauro Vigliano wa Argentina (AVAR 1); Carlos Astroza wa Chile (AVAR2) na Daniele Orsato wa Italia yeye atakuwa AVAR3.
  Nestor Pitana anakuwa mwamuzi wa pili wa Argentina kuchezesha mara mbili michuano ya Kombe la Dunia baada ya Norberto Coerezza, kufanya hivyo mwaka 1970 na 1978.
  Pitana yeye amechezesha fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 huko Brazil ambapo miongoni mwa mechi alizochezesha ni iliyozikutanisha Ufaransa na Ujerumani katika robo fainali.
  Urusi ni moja ya nchi daifu kisoka kwenye mashindano ya mwaka huu, ikiwa inashika nafasi ya 70 kwenye viwango vya shirikisho la soka la kimataifa, lakini wanatarajiwa kucheza vizuri.
  Kocha wa Urusi, Stanislav Cherchesov alikuwa na wachezaji wake wote wakubwa kwenye mazoezi ya mwisho jana kama akina Aleksandr Golovin, Fedor Smolov na Alan Dzagoev.
  Fainali za Kombe la Dunia zinaanza leo kwa mchezo wa ufunguzi wa Kundi A, kati ya wenyeji, Urusi na Saudi Arabia  
  Igor Akinfeev alikuwepo mazoezini pia kama kipa akionyesha uwezo wake mkubwa wa kuokoa kuelekea mchezo wa leo wa ugungzi.
  Urusi wataingia kwenye mchezo wa leo wakitoka kucheza mechi saba mfululizo bila kushinda na Saudi Arabia hawajashinda mechi katika Kombe la Dunia tangu mwaka 1994.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPYENGA CHA KWANZA CHAPULIZWA LEO KOMBE LA DUNIA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top