• HABARI MPYA

  Sunday, June 10, 2018

  KILA LA HERI SIMBA SC….WAPIGENI HAO GOR MAHIA TUPOKEE KOMBE KESHO DAR

  Na Mwandishi Wetu, NAKURU
  BINGWA wa michuano ya SportPesa Super Cup 2018 anatarajiwa kupatikana leo kwa mchezo kati ya wenyeji, Gor Mahia na Simba SC ya Dar es Salaam, Tanzania Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya.
  Simba SC imefika Fainali baada ya kuzitoa Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys za Kenya pi azote kwa penalti baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90, wakati Gor Mahia ilizichapa 3-0 JKU ya Zanzibar na 2-0 Singida United ya Tanzania.
  Baada ya sare ya 0-0 dakika 90, SImba ikaitoa kwa penalti 3-2 Kariobangi Sharks kabla ya kuwatupa nje Kakamega Homeboyz kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 katika Nusu Fainali, kipa wake Aishi Manula ambaye pia ni kipa namba wa Tanzania aking’ara.

  Lakini Simba SC itaendelea kuongozwa na Kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Juma baada ya kukimbiwa na kocha wake, Mfaransa Pierre Lechantre aliyeanza kazi Januari 18 tu, mwaka huu.
  Lechantre na Msaidizi wake aliyekuja naye, Mtunisia Aymen Hbibi Mohammed Alhamisi walikuwa jukwaani wakati Simba SC ikimenyana Simba SC na Kakamega Homeboyz katika Nusu Fainali kabla ya Ijumaa kuondoka kuerejea kwao kufuatia kutofautiana na uongozi chini ya Kaimu Rais wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye yupo Kenya pia.
  Bingwa wa SportPesa Super Cup atapata dola za Kimarekani 30,000 pamoja na nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
  Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500. 
  Gor Mahia ndiye bingwa mtetezi ambaye mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kila la heri Simba SC. Tunataka kupokea Kombe Dar es Salaam kesho. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILA LA HERI SIMBA SC….WAPIGENI HAO GOR MAHIA TUPOKEE KOMBE KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top