• HABARI MPYA

  Friday, June 08, 2018

  KANE ASAINI MKATABA MPYA TOTTENHAM SPURS HADI 2024

  Harry Kane amesaini mkataba mpya wa miaka sita na Tottenham Hotspur 

  KUPANDA KWA MSHAHARA WA KANE 

  AGOSTI 2014 – Pauni 20,000 (hadiu 2019)
  JANUARI 2015 – Pauni 35,000 (hadi 2020)
  DESEMBA 2016 – Pauni 100,000 (hadi 2020)
  JUNI 2018 – Pauni 200,000 (hadi 2022)
  MSHAMBULIAJI Harry Kane amesaini mkataba mpya wa miaka sita na Tottenham ambao utamfanya aongezewe mshahara hadi Pauni Milioni 90 mwa muda wote huo.
  Nahodha huyo wa England amekuwa akilipwa mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki ambao sasa atakuwa analipwa mara mbili na kupokea Pauni Milioni 15 kwa mwaka, akiingia kwenye orodha ya wachezaji wa Ligi Kuu ya England wanaolipwa vizuri.
  Mwenyekiti, Daniel Levy ameendelea na jitihada zake za kuhakikisha anabaki na timu imara kwa kumtia pingu na Kane akitoka kumsainisha mkataba mpya wa miaka mitano kocha  Mauricio Pochettino.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KANE ASAINI MKATABA MPYA TOTTENHAM SPURS HADI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top