• HABARI MPYA

    Sunday, June 03, 2018

    JKU WAREJEA ‘CHOMBO’ KIMOJA NA YANGA SC KESHO BAADA YA KUPIGWA 3-0 NA GOR MAHIA LEO

    Na Mwandishi Wetu, NAKURU
    TIMU ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar imeungana na Yanga kuaga mapema michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuchapwa mabao 3-0 na mabingwa watetezu, Gor Mahia jioni ya leo Uwanja wa Afraha, Nakuru.
    Mabao yaliyoizamisha JKU leo yamefungwa na George Odhiambo, Godfrey Walusimbi na Meddie Kagere na sasa JKU itapanda ndege moja na ndugu zao, Yanga SC kurejea Dar es Salaam kila timu ikipatiwa kifuta jasho cha dola za Kimarekani 2,500 kiasi cha Sh. Milioni 6.
    Mabingwa wa Tanzania, Simba SC wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo, watatupa mguu wao wa kwanza kesho kwa kumenyana na Kariobangi Sharks katika mchezo wa mchana, kabla ya Singida United kumenyana na AFC Leopards jioni.

    Meddie Kagere ameendeleza moto wa mabao Gor Mahia ikiichapa 3-0 JKU leo Nakuru

    Washindi wa mechi hizo watakutana katika Nusu Fainali Juni 7, ya kwanza ikikutanisha washindi wa mechi za leo na ya pili ikikutanisha washindi wa mechi za kesho.
    Na fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Juni 10 na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
    Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKU WAREJEA ‘CHOMBO’ KIMOJA NA YANGA SC KESHO BAADA YA KUPIGWA 3-0 NA GOR MAHIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top