• HABARI MPYA

  Wednesday, June 06, 2018

  DE BRUYNE AMTETEA GUARDIOLA TUHUMA ZA KUBAGUA WAAFRIKA

  KIUNGO Kevin De Bruyne amemtetea Pep Guardiola juu ya madai ya kutowapenda wachezaji Waafrika — kufuatia kocha huyo wa Manchester City kushutumiwa na Yaya Toure na wakala wake.
  Alipoulizwa kiungo huyo wa Man City, De Bruyne juu ya madai ya mchezaji mwenzake wa zamani, Toure, alisema: "Sijawahi kuona kitu chochote. Itakuwa mbaya kama kocha atakuwa anabagua watu weusi kwenye timu yetu.
  "Hivyo, sijui kama Yaya alisema sahihi, ama alikosea  au alikuza mambo. Wakati wowote unapokuwa huchezi unajaribu kutafuta sababu,".

  Kevin De Bruyne amemtetea Pep Guardiola juu ya madai ya Yaya Toure na wakala wake kwamba anawachukia wachezaji weusi 

  "Tumekuwa na msimu mzuri daima, hivyo mwishowe kocha alifanya maamuzi sahihi ya uteuzi wa timu ya kucheza zaidi. Hivyo, mwaka huu kocha alifikiri hakufanya kiasi cha kutosha, hakuwa fiti kiasi cha kutosha. SIjaona kitu cha ubaguzi katika klabu, daima.’
  Lakini siku moja baada ya Toure kumsema kocha wake huyo, wakala wake naye, Dimitry Seluk akaungana naye akisitiza ‘Wachezaji wa Afrika wangeweza kuisaidia City kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Mrusi huyo, Seluk pia amesema kwamba Guardiola hajafikia rekodi ya ushindi wa mataji ya mtangulizi wake Man City, Manuel Pellegrini . 
  ‘Kama Sheik Mansour na Rais Khaldoon Al Mubarak wanafikiri Guardiola anawapenda, wanakosea. Amekwenda pale kuchuma mamilioni ya Mabilionea wa Kiarabu," amesema Seluk. 
  "Guardiola amevuna nini? Ndani ya miaka miwili ameshinda sawa na (Roberto) Mancini au (Manuel) Pellegrini. Pellegrini alifika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa, na Guardiola? Bado.
  "City imemuongezea mkataba kwa miaka mitatu. Napinga Guardiola hatashinda Ligi ya Mabingwa wakati wake (Man City), haijalishi kiasi gani cha fedha ametumia,".
  "Ana chuki na waafrika wote. Mashabiki wengi wa Afrika wamejiondoa Man City. Nina uhakika siku zijazo Waafrika watamzuia Guardiola kushinda taji la Ligi ya Mabingwa,". Hii itakuwa vita ya Guardiola na Waafrika. Maisha yataonyesha kama nipo sahihi,"
  Guardiola jana alisema kwamba: "Siwezi kuzungumzia maneno ya Yaya Toure,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BRUYNE AMTETEA GUARDIOLA TUHUMA ZA KUBAGUA WAAFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top