• HABARI MPYA

  Wednesday, June 13, 2018

  AZAM FC YAIPA PIGO LINGINE SINGIDA UNITED, YAMREJESHA KIKOSINI ‘MIDO FUNDI’ MUDATHIR YAHYA ABBAS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imefanikiwa kumrejesha kiungo wake, Mudathir Yahya kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kutoka Singida United.
  Mudathir, kiungo Mzanzibar hodari leo amesaini mkataba huo mbele ya Makamu Mwenyekiti, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Meneja Philipo Alando.
  Mudathir alikwenda Singida United msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wake Azam na baada ya kazi nzuri akiwa na timu hiyo ya Uwanja wa Namfua amerejeshwa nyumbani.
  Ikumbukwe mchezaji huyo aliibuliwa katika mfumo wa soka ya vijana ya klabu hiyo, maarufu kama Azam Akademi mwaka 2013, kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza – ingawa baadaye ushindani wa namba ukamsukumia nje.
  Mudathir Yahya (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' baada ya kusaini leo
  Mudathir Yahya akisani mkataba wa kurejea Azam FC. Kushoto ni Meneja Philipo Alando

  Mudathir anakuwa mchezaji wa pili kusaini Azam FC kutoka Singida United ndani ya wiki mbili, baada ya Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu na kwa ujumla ni mtu wa tatu kutoka Namfua kuhamia Chamazi, baada ya kocha Mholanzi pia, Hans van der Pluijm.
  Azam pia imewasajili Mzimbabwe mwingine, Donald Ngoma kutoka Yanga SC na mzawa, mshambuliaji Ditram Nchimbi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPA PIGO LINGINE SINGIDA UNITED, YAMREJESHA KIKOSINI ‘MIDO FUNDI’ MUDATHIR YAHYA ABBAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top