• HABARI MPYA

  Monday, June 04, 2018

  AMRI SAID ‘STAM’ AVAA VIATU VYA NDAYIRAGIJJE MBAO FC, AMUACHIA MATOLA LIPULI YAKE

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mbao FC ya Mwanza leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Amri Said ‘Stam’ kuifundisha timu hiyo kwa msimu ujao.
  Mkataba huo umesainiwa leo kwenye ofisi za wadhamini wakuu wa Mbao FC, GF Trucks &Equipment Limited, Vingunguti mjini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Imran Karmali.
  Na ni Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi aliyesaini mkataba huo na Amri Said leo mjini Dar es Salaam.
  Amri Said, beki wa zamani wa Maji Maji ya Songea na Simba SC ya Dar es Salaam anachukua nafasi ya kocha wa muda wa, Fulgence Novatus aliyekuwa anaiongoza timu hiyo baada ya kuondokewa na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Mrundi Etienne Ndayiragijje.
  Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi (kushoto) akipeana mkono na Amri Said baada ya kusaini mkataba leo

  Amri Said (wa kulia) akiwa na viongozi na wafadhili wa Mbao FC leo Vingunguti, Dar es Salaam

  Ndayiragijje ambaye aliiongoza kwa mafanikio Mbao FC kwa msimu mmoja na nusu ikiwemo kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) amejiunga na Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC). 
  Amri anajiunga na Mbao FC akitokea Lipuli ya Iringa ambako alikuwa kocha Msaidizi mbele ya Suleiman Matola mchezaji mwenzake na Nahodha wake wa zamani SImba SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMRI SAID ‘STAM’ AVAA VIATU VYA NDAYIRAGIJJE MBAO FC, AMUACHIA MATOLA LIPULI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top