• HABARI MPYA

  Saturday, May 05, 2018

  YAYA TOURE ATEMWA MAN CITY, ATAAGWA KWA HESHIMA JUMATANO

  Pep Guardiola amethibitisha kwamba Yaya Toure ataondoka baada ya msimu huu Manchester City PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  MAISHA YA YAYA TOURE NDANI YA MANCHESTER CITY  

  Amecheza mechi 315, amefunga mabao 79 na kutoa pasi za mabao 50
  Mataji aliyoshinda:
  Ligi Kuu: 2011/12, 2013/14, 2017/18
  Kombe la FA: 2011
  Kombe la Ligi: 2014, 2016, 2018 
  KIUNGO Yaya Toure tayari ameanza kupiga hesabu za maisha nje ya Manchester City na anatazamiwa kubaki Ligi Kuu ya England baada ya kuambiwa hatapewa mkataba mpya Etihad.
  Pep Guardiola amethibitisha Ijumaa kwamba Muivory Coast huyo atahitimisha miaka yake nane ndani ya klabu hiyo, lakini inaaminika Toure anataka kuendelea kucheza England.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kupewa Unahodha katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Brighton Jumatano na atakabidhiwa zawadi baada ya mechi kuutambua mchango wake katika klabu hiyo. 
  Guardiola pia amesema mchezo dhidi ya Brighton utakuwa maalum wa Toure kuwaaga mashabiki Uwanja wa Etihad.
  "Hatabaki msimu huu,"amesema Guardiola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YAYA TOURE ATEMWA MAN CITY, ATAAGWA KWA HESHIMA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top