• HABARI MPYA

  Monday, May 07, 2018

  SIMBA SC NA NDANDA FC KATIKA PICHA JANA TAIFA

  Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi (kulia) akijivuta kupiga mpira dhidi ya beki wa Ndanda FC, William Lucian 'Gallas' katika mchgezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilishinda 1-0  
  Emmanuel Okwi (kulia) akikimbia na mpira dhidi ya beki wa Ndanda FC, Hemed Khoja 
  Winga wa Simba, Shiza Kichuya (kulia) akitafuta maarifa ya kumpita Jacob Massawe wa Ndanda
  Nahodha wa Simba SC, John Bocco akiutuliza mpira mbele ya Ayoub Masoud wa Ndanda FC  
  Kiungo mshambuliaji wa Ndanda FC, Mrisho Ngassa akimiliki mpira katikati ya wachezaji wa Simba, Jonas Mkude (kushoto) na Erasto Nyoni (kulia)
  Kiungo Mghana wa Simba SC, James Kotei akijaribu kumlamba chenga Omar Mponda wa Ndanda
  Beki Mghana wa Simba, Asante Kwasi akimtoka Jacob Massawe wa Ndanda FC
  Beki wa Ndanda FC, Ayoub Masoud akiteleza chini kuondosha mpira miguuni mwa Shomary Kapombe
  Mmiliki mtarajiwa wa Simba SC, Mohammed Dewji (kushoto) akizungumza jambo na jamaa 
  Wachezaji wa akiba wa Simba, viungo Said Ndemla (kulia) na Muzamil Yassin (kushoto) wakifuatilia mchezo kwa makini
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA NDANDA FC KATIKA PICHA JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top