• HABARI MPYA

  Friday, May 04, 2018

  SHIME KOCHA MPYA KILIMANJARO QUEENS, MSAIDIZI WAKE EDNA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa JKT Tanzania, Bakari Shime ameteuliwa kuwa kocha Mkuu wa kikosi cha timu ya Tanzania Bara(Kilimanjaro Queens) kitakachoshiriki katika mashindano ya Cecafa ya Chalenji kwa Wanawake yatakayofanyika nchini Rwanda.
  Shime atasaidiwa na Edna Lema kocha msaidizi na Eliu Terry kocha wa makipa.
  Kikosi hicho cha Kilimanjaro Queens kinaingia kambini leo kikiwa na wachezaji 25 nkujiandaa na mashindano ya CECAFA Chalenji kwa Wanawake yanayotarajia kuanza Mei 12,2018 nchini Rwanda.
  Kikosi cha Wachezaji 25 kilichoitwa kinaundwa na Sophia Edward Mwasikili wa Kigoma Sisterz, Asha Saada Rashid ‘Mwalala’ wa JKT Queens, Fatuma Mustapha Swalehe wa Jkt Queens, Gelwa Yona Rugomba wa Kigoma Sisterz, Ester Elastus Mayala wa Baobab Queens, Enekia Kasonga Lunyamila wa Alliance Girls, Wema Richard Male wa Mlandizi Queens na Mwanahamis Omari Shurua wa Mlandizi Queens.
  Wamo poia ni Asha Shabani Hamza wa Kigoma Sisterz, Najiat Abass Idrisa wa Jkt Queens, Happiness Hensron Mwaipaja wa Jkt Queens, Maimuna Hamisi Kaimu wa Jkt Queens, Amina Alli Bilali wa Kigoma Sisterz, Donisia Daniel Minja, Jkt Queens, Stumai Abdallah Athumani wa Jkt Queens, Fatuma Issa Maonyo wa Evergreen na Evelina Huobart Sekikubo wa Baobab Queens.
  Wengine ni Rehema Abdu Rhamia wa Kigoma Sisterz, Fatuma Omar Jawady wa Jkt Queens, Christina Daudi Chamwile wa Evergreen, Fatuma Bushiri wa Jkt Queens, Amisa Athuman wa Jkt Queens, Violet Nicholaus wa Kigoma Sisterz, Julieth Singano wa Simba Queens na Fatuma Khatibu wa Jkt Queens.
  Benchi La Ufundi linaongozwa na mwenyewe Bakari Shime, Kocha Msaidizi Edna Lema, kocha wa makipa Eliutery, Neema Msitha, Meneja Easter Chaburuma na Mtunza Vifaa Blandina Manambya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHIME KOCHA MPYA KILIMANJARO QUEENS, MSAIDIZI WAKE EDNA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top