• HABARI MPYA

  Friday, May 04, 2018

  RUVU SHOOTING YAGAWANA POINTI NA MWADUI FC MABATINI, SARE 1-1

  Na Mwandishi Wetu, MLANDIZI
  TIMU ya Ruvu Shooting FC ya Pwani imegawana pointi na Mwadui FC baada ya sare ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani katika mchezo wa Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Mwadui FC waliuanza mchezo huo vizuri kwa bao la mapema la kiungo wake, Abdallah Sesema dakika ya kwanza tu, kabla ya Fully Maganga kuisawazishia Ruvu Shooting dakika ya 69.  
  Kwa matokeo hayo Ruvu Shooting inajiongezea pointi moja na kufikisha 33 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda hadi nafasi ya saba kutoka ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya timu 16, wakati Mwadui FC inabaki katika nafasi ya tisa kwa pointi zake 30 za mechi 27 pia. 
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Singida United FC wakiikaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Namfua na Tanzania Prisons FC wakiwa wenyeji wa Lipuli FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Na Jumapili Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wenyeji Maji Maji wataikaribisha Mtibwa Sugar, Kagera Sugar FC wataikaribisha Mbeya City FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Stand United FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Simba SC watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAGAWANA POINTI NA MWADUI FC MABATINI, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top