• HABARI MPYA

  Thursday, May 03, 2018

  NI LIVERPOOL NA REAL MADRID FAINALI LIGI YA MABINGWA MEI 26 KYIV

  Sadio Mane akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Liverpool dakika ya tisa wakifungwa 4-2 na wenyeji, Roma katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Olimpiki mjini Roma. Bao la pili la Liverpool inayokwenda kwa fainali kwa ushindi wa jumla wa 7-6 baada ya kushinda 5-2 kwenye mechi ya kwanza, lilifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 25, wakati mabao ya Roma yalifungwa na  James Milner aliyejifunga dakika ya 15, Edin Dzeko dakika ya 52, Radja Nainggolan dakika ya 86 na 90 na ushei kwa penalti. Liverpool itakutana na Real Madrid iliyoitoa Bayern Munich katika fainali itakayofanyika Mei 26, mwaka huu Uwanja wa NSK Olimpiki mjini Kyiv, Ukraine PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI LIVERPOOL NA REAL MADRID FAINALI LIGI YA MABINGWA MEI 26 KYIV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top