• HABARI MPYA

    Wednesday, May 02, 2018

    NGORONGORO HEROES YAENDELEA VIZURI NA MAANDALIZI, KUIVAA MALI MEI 13 TAIFA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Mali U20 Jumapili Mei 13,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo utakaochezwa saa 10:00 jioni kiingilio cha kuingia Uwanjani kutazama mechi hiyo VIP zote shilingi 3,000 Mzunguko shilingi 1,000.
    Ngorongoro Heroes wapo kambini wakiendelea kujiandaa na mchezo huo,leo wapo kwenye ratiba ya kufanya mazoezi ya gym asubuhi na jioni kabla ya kuwa na mazoezi ya uwanjani kesho na Ijumaa ambapo kesho Alhamisi watakuwa na kipindi kimoja cha Uwanjani saa 10 kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ijumaa watafanya vipindi viwili asubuhi na jioni saa 10.

    Kocha wa Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje anawaandaa vijan awake kuikabili Mali Mei 13

    Kikosi hicho hakina majeruhi vijana wana morali kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu fainali za vijana Afrika.
    Ikifanikiwa kuitoa Mali, itakutana na mshindi kati ya Uganda na Cameroon katika hatua ya mwisho ya mchujo wa fainali za mwakani za U20.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAENDELEA VIZURI NA MAANDALIZI, KUIVAA MALI MEI 13 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top