• HABARI MPYA

  Friday, May 04, 2018

  MSUVA AKUTANA NA YANGA ALGERIA KWA AJILI YA MECHI ZA UFUNGUZI HATUA YA MAKUNDI MICHUANO YA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva atakutana na klabu yake ya zamani, Yanga SC mjini Algiers leo.
  Msuva yupo Algiers na klabu yake, Difaa Hassan El- Jadidi kwa ajili ya mchezo wao wa ufunguzi hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Mouloudia Club D'Alger Saa 4:00 usiku wa leo.
  Na Yanga wanawasili mjini humo leo kwa ajili ya mchezo wao wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M. Alger utakaofanyika Jumapili.
  Simon Msuva atakutana na klabu yake ya zamani, Yanga SC mjini Algiers leo

  Msuva yupo katika msimu wake wa kwanza tu Difaa Hassan El- Jadidi tangu ajiunge nayo Juni mwaka jana kutoka kwa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga SC.  
  Na Msuva timu yake imepangwa Kundi B pamoja na Mouloudia Club D'Alger, E. S. Setifienne ya Algeria na TP Mazembe ya DRC.
  Yanga na U.S.M. Alger zipo Kundi D pamoja na Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya ambazo zitamenyana zenyewe katika ufunguzi wa hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
  Baada ya mechi ya kwanza ugenini Jumapili, Yanga itamenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
  Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AKUTANA NA YANGA ALGERIA KWA AJILI YA MECHI ZA UFUNGUZI HATUA YA MAKUNDI MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top