• HABARI MPYA

  Saturday, May 05, 2018

  JOSHUA: NITAPIGANA NA HAYE KAMA ATALIPA KISASI KWA BELLEW

  BONDIA Anthony Joshua amefungua milango kwa ya pambano kubwa la ngumi za kulipwa uzito wa juu duniani na David Haye, ikiwa Hayemaker atashinda pambano la marudiano na Tony Bellew usiku wa Jumamosi.
  Mbabe huyo anayeshikilia mataji yote ya uzito wa juu duniani kasoro moja tu, yupo kwa majadiliano ya ofa ya dola za Kimarekani Milioni 50 kupigana na bingwa wa WBC, Deontay Wilder, lakini atakuwa tayari kupigana na Haye kwanza kama dili hilo litaendelea kusuasua.
  Haye amemjibu Joshua kwa kusema: "Anaweza kupata hiyo kazi na mimi. Ikiwa yeye au Wilder wako siriasi wanaweza kupata hilo pambano, hakuna tatizo,".

  Anthony Joshua amefungua milango ya pambano kubwa la ngumi uzito wa juu duniani dhidi ya Muingereza mwenzake, David Haye PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Pambano kati ya Joshua na Haye linaweza kuujaza Uwanja wa Wembley siti zake zote 90,000 likitokea.
  Joshua atakuwa pembezoni mwa ulingo ukumbi wa 02 kumuangalia Haye kama atalipa kisasi cha kipigo cha mwaka jana cha Bellew.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA: NITAPIGANA NA HAYE KAMA ATALIPA KISASI KWA BELLEW Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top