• HABARI MPYA

    Thursday, May 03, 2018

    BEKI MGHANA WA AZAM FC APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa kati wa Azam FC, Yakubu Mohammed ameondoka leo mchana mjini Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kwa matibabu ya kifundo cha mguu.
    Meneja wa Azam FC, Philipo Alando ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Mohammed atafanyiwa ufunguzi kesho Saa 4:00 asubuhi katika hospitali ya iliyopo mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
    Alando amesema mchezaji huyo amekuwa nje ya Uwanja tangu Machi kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu na pamoja na kufanyiwa matibabu ikiwa ni pamoja na kufungwa Plasta Gumu (PoP), lakini hajapata nafuu.
    Yakubu Mohammed amekwenda Afrika Kusini leo kwa matibabu ya kifundo cha mguu 

    “Yakubu ana mpasuko kwenye mfupa wa kifundo cha mguu, alitibiwa mwezi wa tatu, lakini hajapata nafuu, sasa ndiyo tunampeleka tena Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi, ili tujue hatua inayofuata,”amesema Alando. 
    Mohammed ameondoka nchini akiongozana na Daktari Mkuu wa klabu, Mwanandi Mwankemwa ambaye ndiye atasimamia matibabu yake huko.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI MGHANA WA AZAM FC APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top