• HABARI MPYA

  Wednesday, April 18, 2018

  VIINGILIO SIMBA NA YANGA MEI 29 TAIFA NI KUANZIA SH. 7,000 HADI 30,000 KWA VIP A

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetaja viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Mei 29 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika Saa 10:00 jioni, kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 7,000 wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.
  Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)
  Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa kupitia Selcom
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIINGILIO SIMBA NA YANGA MEI 29 TAIFA NI KUANZIA SH. 7,000 HADI 30,000 KWA VIP A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top